Simba yaitangazia kiama Wydad

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Dec 2023
Simba yaitangazia kiama Wydad

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally leo ametangaza viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wydad ambao utapigwa Jumanne, Disemba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Tiketi za mchezo huo zinauzwa sambamba na tiketi za mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Uhuru

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Ahmed alisema Simba inahitaji tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa hivyo Wydad wafahamu wanakwenda kukutana na moto pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Ahmed amewataka mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi dimba la Mkapa kwaani pasipo uwepo wao malengo yao yanaweza yasifanikiwe

"Kufika robo fainali tutafanikisha kwa kila Mwanasimba kuhusika kwa kuja uwanjani. Malengo yetu ni nusu fainali na itakuwa aibu kubwa sana tusipofika robo fainali. Na Simba ya sasa nyie wenyewe mnaiona, timu ina mabadiliko makubwa"

"Wydad watakutana na moto wa volcano, siku hiyo lazima wakae na tushinde. Mechi hiyo inawahitaji zaidi Wanasimba. Ni mechi yakutengeneza njia ya kwenda robo fainali, Simba sio timu ya kuishia hatua ya makundi"

"Viingilio vya mchezo dhidi ya Wydad; Mzunguko - Tsh. 5,000. VIP C - Tsh. 10,000. VIP B - Tsh. 20,000. VIP A - Tsh. 30,000. Platinum - Tsh. 150,000"

"Mgeni rasmi atakuwa mwalimu Abdelhak Benchikha 'GENERAL'. Yeye ndio tumempa hadhi hiyo. Huyu ndio kocha bora wa Afrika kwa vilabu na kocha wa tatu kwa ubora Afrika lakini pia ni mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika tukiwa nyumbani na sababu kuu ni mabadiliko ambayo ameyaleta"

"Huyu ni kocha mkubwa sana Afrika, Wanasimba tujivunie tukiwa ba kocha Abdelhak Benchikha. Ndugu yangu Mwanasimba na wewe hakikisha unaandika historia siku hiyo kuwepo uwanjani," alisema

Aidha Ahmed alibainisha kuwa watafanya hamasa kubwa kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha Wanasimba wanajitokeza kwa wingi kujaza uwanja wa Mkapa

"Tuna mpango wa kufanya hamasa kubwa ambayo haijawahi kutokea. Uzinduzi utafanyika tarehe 16 Desemba, 2023 eneo ni Mbagala Zakhem. Msafara utaanzia Uwanja wa Mkapa na magari kama 2,000."

"Katika uzinduzi kutakuwa na burudani nyingi kutoka kwa King Faida, Doto na balaa kubwa zaidi litasindikizwa na Miso Misondo."

Kaulimbiu ya mchezo huo ni "HAIJAKWISHA HADI IISHE. It's not over until it's over."

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
5h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
7h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
8h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
8h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
9h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
14h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
15h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
15h ago
READ MORE β†’