Yanga ina historia ya kipekee na visiwa vya Zanzibar na haishangazi nyota wanaosajiliwa kutoka visiwa Zanzibar hun'gara zaidi wakicheza Yanga kuliko klabu nyingine Tanzania Bara
Imekuwa sehemu ya utamaduni wa Yanga katika kila dirisha la usajili kuongeza fundi angalau mmoja kutoka visiwani Zanzibar
Chanzo kisicho na shaka kimebainisha kuwa Yanga tayari imekamilisha usajili wa kiungo Shekhan Ibrahim Khamis anayeitumikia klabu ya JKU
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji anatajwa kufanikisha usajili wa kiungo huyo anayemudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji
Kulikuwa na vigogo wengine kutoka jijini Dar es salaam waliokuwa wakimuwania Shekhan (18) lakini wameshinda vita ya kumsajili kiungo huyo ambaye usajili wake ulikamilishwa mapema Jumatano jijini Dar es salaam
Shekhan amepewa kandarasi ya Miaka mitatu kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara