Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Disemba 08 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Dec 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Disemba 08 2023

Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 31, mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 30, na winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, huku meneja Erik ten Hag akijaribu kupunguza kikosi chake. (Independent)

Beki wa kati wa Everton Jarrad Branthwaite, 21, na mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, 23, wako kwenye orodha ya watu wanaosakwa na Ange Postecoglou huku mkufunzi huyo wa Tottenham akiunda upya kikosi cha klabu hiyo. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Everton Dele Alli, 27, anakaribia kurejea kwenye mazoezi kamili huku akiongeza ahueni ya jeraha la paja ambalo limemaanisha kuwa bado hajacheza msimu huu. (Times – Subcription Required)

Fulham watamlenga kiungo wa kati wa Brazil Andre, 22, kutoka klabu ya Fluminense iwapo iwapo kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, ataondoka Craven Cottage mwezi Januari. (Telegraph – Subscription Required)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumsajili Palhinha kutoka Fulham hatua ambayo itakuwa muda wa mwish wa kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey mwenye umri wa miaka 28 na The Gunners. (Mirror)

Manchester United na Newcastle sasa wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Guinea Serhou Guirassy, 27 kutoka Stuttgart. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, atasusia kuhamia Ligi ya Premia na kutia saini mkataba mpya na Juventus. (Gazzetta Dello Sport – In Italy)

Inter Milan wamepanga kuvunja mfumo wao wa mishahara ili kumsainisha mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 26, kwenye mkataba mpya wa muda mrefu. (Calciomercato – In Italy)

Lyon wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Rayan Cherki mwenye umri wa miaka 20 mwezi Januari huku West Ham na Chelsea wakimtaka. (Footmercato – In French)

Fowadi wa Ujerumani Timo Werner ameambiwa na mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Rouven Schroder kwamba anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo mwezi Januari, lakini si Manchester United wala Real Madrid wana uwezezo wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Bild – In Deutsch)

Fowadi wa Uhispania Ferran Torres, 23, amemwambia meneja wa Barcelona Xavi kwamba amejitolea kuitumikia klabu hiyo na hataki kuondoka Januari. (Mundo Deportivo – In Spanish )

Sunderland wanamhoji kocha wa Sweden Kim Hellberg, ambaye amesema anaondoka IFK Varnamo, kuhusu kuwa meneja wao baada ya kutimuliwa kwa Tony Mowbray. (Times – Subscription Required)

Beki wa Uhispania Jonny Otto, 29, ana mazungumzo yanayoendelea na Wolves kuhusu hatma yake huko Molineux baada ya tukio la hivi majuzi la uwanja wa mazoezi. (Express & Star – Subscription Required)

Kipa wa Ufaransa Mike Maignan, 28, anafikiria hatma yake katika klabu ya AC Milan baada ya mazungumzo ya kandarasi kukwama, huku Chelsea, Bayern Munich na Paris St-Germain zote zikifuatilia maendeleo yake. (Dakika 90)

Real Madrid wamemtambua Alphonso Davies wa Bayern Munich kama suluhu lao la muda mrefu katika nafasi ya beki wa kushoto, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na wasiwasi kuwa haitaweza kutimiza matakwa ya mshahara wa mlinzi huyo wa Canada mwenye umri wa miaka 23 katika siku zijazo. (Mundo Deportivo - Spanish)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’