Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Disemba 06 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Dec 2023
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Disemba 06 2023

Timu ya Bayern Munich itakabiliana na ushindani kutoka vilabu viwili vya Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa kumnunua kiungo wa Fulham na Ureno, Joao Palhinha (28), mwezi Januari - limeandika gazeti la Telegraph

Bayern wanaweza kumkosa kiungo wa kati wa Bayefdcer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz pia, kwani Manchester City na Liverpool zina nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, mtandao wa 90min unaeleza

Mshambulizi wa Gremio na Uruguay, Luis Suarez (36), anatazamiwa kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami kwa mkataba wa mwaka mmoja. (Miami Herald)

Kocha wa zamani wa Wolves, Julen Lopetegui alikataa kandarasi ya pauni milioni 15.4 za Uingereza kwa msimu kutoka kwa timu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia akitaka kusalia kwenye Ligi ya Kuu ya Uingereza, huku Manchester United ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa kutaka kumwajiri Mhispania huyo. (AS)

Kitahitajika kitita cha pauni milioni 60 kwa Aston Villa kufikiria kumuuza Douglas Luiz ifikapo mwezi Januari, huku Arsenal ikionyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Caught Offside)

Arsenal na Liverpool zote zilituma mawakala kumtazama beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong (22). (90min)

Real Sociedad wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza, Mason Greenwood (22), ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe. (Todofichajes)

Donny van de Beek wa Manchester United amejitoa kwa Barcelona, kiungo huyo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 - anatumai ataziba pengo la kuumia Gavi. (Sport)

Wakati huo huo, Manchester United inatazamiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund na Uholanzi, Donyell Malen (24), ikiwa winga wa Uingereza, Jadon Sancho (23), ataondoka katika klabu hiyo. (Football Transfers)

Wolves wanavutiwa na beki wa pembeni wa Sevilla na Argentina, Marcos Acuna (32), anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni za Uingereza milioni 10.3. (Todofichajes)

Timu ya Sao Paolo wako tayari kumuuza mchezaji anayelengwa na Liverpool, Lucas Beraldo, wakati Wolves ilikataliwa ombi la kumnunua mlinzi huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 20 msimu wa joto. (90min)

Juventus wako tayari kumwachia winga wa Uingereza, Samuel Iling-Junior kuondoka mwezi Januari huku Tottenham na Newcastle wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Tuttomercatoweb)

West Ham, Everton, Brighton na vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uingereza viko katika kinyang'anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Linfield mwenye umri wa miaka 17 na Ireland Kaskazini, Aodhan Doherty. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
6m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
57m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’