Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Novemba 14 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Novemba 14 2023

Mshambuliaji wa Tottenham na Brazil Richarlison, 26, na winga wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho, 23, wanawaniwa na klabu za Ligi Kuu ya Saudia. (Telegraph - usajili unahitajika)

Juventus pia wana hamu ya kumsajili Sancho lakini kwa mkopo huku wakitarajia United kulilipa sehemu ya mshahara wake. (Fabrizio Romano)

Hata hivyo, United hawako tayari kumwachilia Sancho kuondoka katika uhamisho wa Januari . (Football Insider)

Real Madrid imewaongeza kiungo wa Ujerumani Florian Wirtz, 20, mlinzi wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 22, na mshambuliaji wa Nigeria Victor Boniface, 22, kutoka Bayern Leverkusen kwenye orodha yao fupi ya uhamisho. (Football Transfers)

Barcelona bado wanapania kumuuza winga wa zamani wa Leeds United Raphinha, 26, msimu ujao, na wanatumai klabu kubwa za Uropa zitaweka dau la kumnunua mshambuliaji huyo wa Brazil. (Fichajes - kwa Kihispania)

Real Madrid wako tayari kumuongezea mkataba mlinzi wa Brazil Eder Militao mwenye umri wa miaka 25 hadi angalau 2028. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Brighton wamemleta mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 19, sambamba na wachezaji wengine wanaolipwa pesa nyingi katika klabu hiyo na kandarasi yake mpya ya miaka sita. (Football Insider)

Rais wa Bayern Munich Herbert Hainer anasema hawana nia ya kumuuza beki wa Canada Alphonso Davies, 23, licha ya tetesi kwamba Real Madrid wanamtaka. (90 Min)

Raia wa Croatia na meneja wa zamani wa Marseille Igor Tudor, 45, anapendekezwa kuchukua nafasi ya Mfaransa Rudi Garcia mwenye umri wa miaka 59 kama kocha wa Napoli. (Fabrizio Romano)

Beki wa zamani wa Italia mzaliwa wa Naples, Fabio Cannavaro, 50, pia yuko kwenye orodha ya wale wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Garcia. (Mail)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
7h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
9h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
10h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
10h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
11h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
14h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
16h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
17h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
17h ago
READ MORE β†’