Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Novemba 09 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Novemba 09 2023

Mshambuliaji wa England Eberechi Eze, 25, anakaribia kukubali kandarasi mpya ya pauni 100,000 kwa wiki katika klabu ya Crystal Palace baada ya kuafikiana kimsingi na klabu hiyo (Mail)

Bayer Leverkusen inasisitiza kuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz, 20, hataondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga mwezi Januari, huku mkurugenzi mkuu Simon Rolfes akikana kuwa Liverpool tayari wamewasilisha ombi la pauni milioni 85.. (Kicker - Kwa Kijerumani)

Mshambuliaji wa Uingereza Jadon Sancho, 23, anatarajiwa kuondoka Manchester United mwezi Januari (Fabrizio Romano)

Real Madrid hawana mpango wa kumsajili fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, hata iwapo ataamua kutoongeza mkataba wake na Paris St-Germain na kuondoka bila malipo msimu ujao. (Cadena SER - kwa Kihispania)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe ana nia yakuimarisha safu yake ya kati katika dirisha la uhamisho la Januari, huku Kalvin Phillips wa Manchester na Muingereza, 27, na Mchezaji wa kimataifa wa Ureno wa Al-Hilal Ruben Neves, 26, wakimfaa katika mipango yake (The I)

Manchester United italazimika kufanya mikataba ya bei ya chini au ya mikopo katika dirisha la usajili la Januari huku kukiwa na sintofahamu juu ya umiliki wao. (Mail)

Tottenham wana nia ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Uingereza Marcus Edwards, ambaye alipitia chuo chao cha mafunzo ya chipukizi na sasa anachezea klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno. Lakini Chelsea pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Correio de Manha - kwa Kireno)

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Argentina Hernan Crespo, 48, anatazamiwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Ain inayoshiriki Ligi ya UAE. (Mail)

Bayern Munich watapambana na Arsenal katika harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi, 24, kutoka Real Sociedad (Bild, kupitia Mirror)

Barcelona wanasalia nyuma ya meneja wao Mhispania Xavi, 43, licha ya klabu hiyo kushuhudia kudorora kwa hali ya mchezo wao. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Casemiro, 31, analengwa Januari na Saudi Pro League. (90min)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
1h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
3h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
4h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
5h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
10h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
11h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’