Gomez aibukia Botswana

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Oct 2023
Gomez aibukia Botswana

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Didier Gomes da Rosa amepata ajira ya kuinoa timu ya taifa ya Botswana

Kocha huyo raia wa Ufaransa, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu ya Taifa ya Botswana na jukumu lake kubwa litakuwa ni kuiongoza timu hiyo kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, zitakazofanyika Morocco

Habari za uhakika kutoka Botswana zinaeleza kuwa Gomes tayari ameshaanza kazi ya kuinoa timu hiyo na kibarua chake cha kwanza kitakuwa ni mechi mbili za kuwania kufuzu fainali Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Msumbiji na Guinea ambazo watacheza mwezi ujao

Kocha huyo ambaye bado hajatambulishwa rasmi na Chama cha Soka Botswana (BFA) katika majukumu yake hayo mapya atasaidiwa na kocha wa zamani wa Township Rollers ya nchini humo, Romain Folz

Da Rosa anakumbukwa nchini kwa kuiongoza Simba kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/2021, ambao iliondoshwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa kufungwa mabao 4-3 katika mechi mbili baina yao

Katika kipindi chake ndani ya Simba, Da Rosa alishinda taji moja la Ligi Kuu, Ngao ya Jamii pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam.

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
1h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
3h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
4h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
10h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
11h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’