Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Oktoba 12 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi, Oktoba 12 2023

Barcelona wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Italia Jorginho, 31. (Mirror)

Jesse Lingard ameongeza nafasi yake ya kuhamia klabu ya Al-Ettifaq ya Saudi Arabia baada ya kuifungia timu ya Steven Gerrard katika mechi ya kirafiki siku ya Jumatano

Mshambuliaji huyo wa Uingereza, 30, amekuwa hana klabu tangu alipoondoka Nottingham Forest msimu huu wa joto. (Goal)

Chelsea wamemuongeza mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, kwenye orodha ya walengwa wa uhamisho wa Januari. (ESPN)

Bosi wa Bayer Leverkusen Mhispania Xabi Alonso, 41, ana kipengele katika mkataba wake ambacho kitamruhusu kuwa meneja wa klabu zake zote za zamani - Liverpool, Real Madrid au Bayern Munich - mapema msimu ujao wa joto. (Bild, Via Mail )

West Ham, Brighton, Crystal Palace na Bournemouth wanavutiwa na mshambuliaji wa Stuttgart na Guinea Serhou Guirassy, 27, ambaye ndiye mfungaji bora wa Bundesliga hadi sasa msimu huu. ( 90 min)

Manchester United wanatazamiwa kuongeza kandarasi za beki wa pembeni wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 25, na mlinzi wa kati wa Sweden Victor Lindelof, 29, lakini itachukua muda wao kabla ya kuamua mustakabali wa fowadi wa Ufaransa Anthony Martial, 27. (ESPN)

Kocha wa zamani wa Tottenham Antonio Conte amekataa nafasi ya kuwa meneja ajaye wa Napoli, huku Muitaliano huyo, 54, akipendelea kusubiri nafasi kwingine. (Fabrizio Romano)

Juventus wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport – In Italy)

Inter Milan wanalenga kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 28. (Calciomercato - in Italy)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 26, anataka kuondoka Aston Villa baada ya kutofautiana na meneja Unai Emery. (Football Insider)

Barcelona inamfuatilia kiungo wa kati wa Porto Muargentina Alan Varela, 22, Royal Antwerp na kiungo wa kati wa Ubelgiji chini ya umri wa miaka 21 Arthur Vermeeren, pamoja na Bayer Leverkusen na Mjerumani Florian Wirtz, 20, huku wakipania kuimarisha safu yao ya kiungo msimu ujao. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Arsenal pia wanavutiwa na Vermeeren, 18, ambaye thamani yake ni takriban £15m. (Team Talks) Bosi wa zamani wa Paris-St Germain Christophe Galtier, 57, anakaribia kuwa meneja mpya wa klabu ya Al-Duhail ya Qatar. (Fabrizio Romano)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
50m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’