Azam Fc imetakata uwanja wa Azam Complex ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida FG katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Alikuwa Iddi Selemani Nado aliyepeleka Singida dakika za jioooni akifunga bao la ushindi ulioipa Azam Fc alama tatu muhimu zinazowafanya wafikishe alama tisa na tofauti ya mabao saba wakifungana na Simba katika nafasi ya pili
Walikuwa Azam Fc waliotangulia kufunga kupitia Cheikh Sidibe aliyefunga kupitia mpira wa adhabu kwenye dakika ya 10
Azam Fc walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili Singida FG wlairekea wakiwa imara na wakafunga bao la kusawazisha kupitia Marouf Tchakei aliyeachia kombora kali kutoka nje ya 18
Ulikuwa mchezo mzuri wa wazi timu hizo zikishambuliana kwa zamu lakini ni Azam Fc walioibuka kidedea baada ya dakika 90