Yanga yaipigia hesabu kali KMC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Aug 2023
Yanga yaipigia hesabu kali KMC

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Azam Complex

Licha ya kutopata muda wa kutosha wa maandalizi baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc, Gamondi amesema wanafahamu aina ya mchezo wanakwenda kukabiliana nao

"Ratiba sio rafiki sana kwa sababu tumecheza Jumapili, lakini kama timu kubwa tunapaswa kujiandaa na kupata matokeo mazuri katika kila mechi"

"Nimewaona KMC kwenye mchezo wao waliocheza Jumamosi (dhidi ya Namungo), ni timu nzuri natarajia utakuwa mchezo mzuri"

"Naamini kwa umoja wetu na sapoti ya mashabiki tutakuwa na mchezo mzuri utakaoambatana na soka safi la ushindani," alisema Gamondi

Kuhusu hali za wachezaji baada ya mchezo dhidi ya Asas Fc, Gamondi amesema baadhi walipata changamoto ndogo lakini anaamini baada ya mazoezi ya mwisho leo watakuwa tayari kwa mchezo huo

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, winga Denis Nkane amesema baada ya kupoteza Ngao ya Jamii, jukumu lao wachezaji ni kuhakikisha wanaanza vyema msimu ili kutetea mataji yote yaliyobaki

Nae Kocha wa KMC Abdilhamid Moalin amesema wametoka kucheza mechi ngumu dhidi ya Namungo Fc na wanakabiliwa na mechi nyingine ngumu dhidi ya Yanga

Moalin amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo lakini watapambana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

KMC ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
2h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
2h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
2h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
3h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
5h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
17h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
19h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
20h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
21h ago
READ MORE β†’