Kikosi cha Simba leo kinaingia siku ya tatu katika kambi ya pre-season inayoendelea huko Uturuki
Ni kambi ya wiki tatu ambayo benchi la ufundi linaitumia kutengeneza kikosi cha maangamizi matumaini ya Wanasimba kuona timu yao inashinda kila taji katika michuano yote watakayoshiriki msimu ujao
Program za mazoezi ziko chini ya makocha Ouanane Sellami na Corneille Hategekimana wakati kocha mkuu Robertinho Oliveira akirejea kwao Brazil kuhudhuria kozi fupi ya masomo ya ukocha (FIFA Pro License)
Mratibu wa Simba Abbas Ally amesema Robertinho aliandaa program yote ya mazoezi hivyo kuondoka kwake hakuwezi kuathiri maandalizi yao
"Kambi yetu iko vizuri, morali ya wachezaji iko juu. Tunafurahi kuona kadiri siku zinazvyoenda wanazidi kushika mafunzo wanayopewa," alisema Abbas