Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Juni 27 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Juni 27 2023

West Ham wamepokea ofa rasmi kutoka kwa Manchester City ili kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24, katika mkataba wa thamani ya hadi £90m. (The Athlete)

Tottenham wanajiandaa kuwasilisha ofa ya ufunguzi ya £40m kwa mchezaji wa Leicester James Maddison - lakini Foxes wanataka pauni milioni 60 kwa nyota wao wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26. (Telegraph – Subscription Required)

Taarifa ya Napoli kukataa nia ya euro 100m ya Paris St-Germain kumnunua mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen mwenye umri wa miaka 24 inaweza kuibua mnada - huku Liverpool, Manchester United na Newcastle zikiwa tayari kutoa ofa. (Gazzetta dello Sport – In Itali)

Bayern Munich wanaweza kuwa mbele ya foleni ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 29, ambaye anasemekana kutaka kuhamia Ujerumani. (Sky Sport Germany)

&Newcastle wako kwenye mazungumzo ya juu na Southampton iliyoshuka daraja kuhusu mkataba unaowezekana wa pauni milioni 15 kwa beki wa pembeni wa Uingereza Tino Livramento, 20. (Telegraph – Subscription Required)

Wachezaji wa Uingereza Jadon Sancho na Harry Maguire ni miongoni mwa wachezaji 13 ambao Manchester United wako tayari kuwauza msimu huu wa joto. (Mail)

Msako wa muda mrefu wa Manchester United wa kumnasa Adrien Rabiot unaweza kupata pigo tena kwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 kusaini mkataba mpya na miamba wa Serie A Juventus. (Corriere dello Sport – In Italy)

Mohamed Salah hataondoka Anfield hivi karibuni licha ya uvumi unaomhusisha fowadi huyo wa Misri na Liverpool, 31, na uhamisho wa kwenda Saudi Arabia. (Mirror)

Hata hivyo, mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool ambaye hana mkataba Alex Oxlade-Chamberlain, 29, anajadili iwapo atakubali ofa nono ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kimataifa wa Uingereza kujiunga na Saudi Pro League. (Mail)

Arsenal wanampanga Youssouf Fofana, 24, kama mbadala wa kiungo wa kati wa West Ham Muingereza Declan Rice, lakini The Hammers na Newcastle pia wanamwinda kiungo huyo wa kati wa Monaco na Ufaransa. (L'Equipe – In French, Subscription Required )

AC Milan Itamsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 27, kutoka Chelsea kwa euro 15m. (Calciomercato – In Itali)

Mkufunzi wa Aston Villa Unai Emery anatamani kuungana tena na beki wa kati wa Villarreal Mhispania Pau Torres, 26, ambaye atagharimu chini ya kifungu chake cha pauni milioni 51.5 hivi majuzi huku mkataba wake ukisalia mwaka mmoja pekee. (Times - Subscription Required )

Sheffield United iliyopanda daraja iko kwenye mazungumzo "ya kina" kumsajili beki wa kati Muingereza Mason Holgate, 26, kwa mkopo kutoka kwa wapinzani wao wa ligi ya Premier Everton. (talkSPORT)

Liverpool wameungana na Arsenal katika mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, kutoka Southampton iliyoshuka daraja. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Wolfsburg ya Bundesliga itahitaji pauni milioni 26 kumnunua mlinzi wa Uholanzi chini ya umri wa miaka 21 Micky van de Ven, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham. (Evening Standard)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
50m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’