Mlinda lango wa Simba Aishi Manula amekamilisha awamu ya kwanza ya matibabu yake Afrika Kusini ambapo alifanyiwa upasuaji
Manula aliruhusiwa kutoka Hospitalini jana na anatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Jumapili
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Simba, Manula atakuwa nje kwa takribani miezi minne akiendeleza kuuguza jeraha
Daktari wa Simba Dk Edwin Kagabo amesema awamu ya pili ya matibabu ya Manula itahusisha kliniki maalum ya mazoezi ambayo itamsaidia kupona jeraha katika muda atakaokuwa nje
ADVERTISE HERE