Singida BS kujipanga upya baada ya kipigo cha Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2023
Singida BS kujipanga upya baada ya kipigo cha Yanga

Baada ya kukishuhudia kikosi chake kikichezea Bakora 2-0 mbele ya Mabingwa watetezi Tanzania Bara Young Africans, Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans van der Pluijm, amesema hatakubali tena kufungwa na wababe hao wa Jangwani

Singida Big Stars Jumatano (Mei 04) ilishindwa kufurukuta katika Uwanja wake wa Nyumbani CCM Liti kwa kukubali kupigwa kichapo hicho ndani ya dakika 20 za kipindi cha kwanza, na kupelekea kuzitema alama tatu muhimu

Pluijm amesema kwenye mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho la Azam 'ASFC' hatakubali kikosi chake kupoteza tena mbele ya Young Africans, kwa sababu atahakikisha anajipanga vizuri ili kushinda mchezo huo na kutinga Fainali ya michuano hiyo.

Amesema hata ikitokea anatinga Fainali ya michuano hiyo, pia hatakuwa tayari kupoteza mbele ya Simba SC au Azam FC ambapo moja kati ya timu hizo itaingia Fainali baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya ASFC utakaochezwa leo Jumapili (Mei 07) mjini Mtwara

"Tulijipanga kushinda mechi zote mbili dhidi ya Young Africans, ila kwa kuwa tumefungwa huu hatutakubali kufungwa kwenye mchezo ujao tena, maana hamu yetu ni kuhakikisha tunacheza na fainali iwe na Simba au Azam atakae ingia," amesema Plujm

Young Africans na Singida BS zitachuana May 21 katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mchezo ambao uliahirishwa na TFF ili kuipa Yanga nafasi ya kujiandaa na mchezo Shirikisho CAF dhidi ya Malumo Gallants

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
4h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
6h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
7h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
8h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
8h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
11h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
13h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
14h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
14h ago
READ MORE β†’