Wadhamini chachu kufanya vizuri Kimataifa - Arafat

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Mar 2023
Wadhamini chachu kufanya vizuri Kimataifa - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema kukua kwa nguvu za kiuchumi kwa klabu za Simba na Yanga imekuwa chachu kwa miamba hiyo ya soka la Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa

Arafat amesema hayo kwenye mjadala wa Simba, Yanga kufuzu robo fainali ya michuano ya kimataifa nini maana yake kwa soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki ambao umechukua nafasi kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ya Mwananchi.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mmoja wa wachangiaji, alianza kwa kupongeza kufuatia uwepo wa mjadala huo ambao umewakutanisha pamoja wadau wa Simba na Yanga kisha kusema;

"Nini kimeibeba Simba na Yanga, Wadau wamekuwa na mchango kwa maana ya kuingia kama wabia, tumeona Yanga wameenda kwa SportPesa na Simba kwa M-Bet huku wakiwemo wengine"

"Hii ni faida ambayo naamini imechangia kwa timu hizi kufika mbali, mpira wa Afrika kuendesha ni ghamara kubwa sana, ili uendelee kuwa imara inahitaji kuwa sawa kiuchumi"

"Timu zetu zimeenda mbali kwa kuwa na mabenchi mapana kwa kuwa na kila mtu na eneo lake tofauti na zamani ambapo mtu mmoja alikuwa akifanya vitu vingi kwa wakati mmoja, zamani tulikuwa tukiona DR Congo ikifanya vizuri lakini kwa sasa imekuwa tofauti inamaana ya kuwa nguvu ya timu zetu kiuchumi zimekua," alisema Arafat

"Tumeona Simba wamemtoa Sakho (Pape) na kwenda timu ya taifa la Senegal, hata kwa Yanga kuna mchezaji kutoka Mali (Diarra), wachezaji mataifa makubwa kwa sasa wanahamasika kucheza hapa, hili inatakiwa kuleta changamoto kwa wachezaji wetu wazawa"

Hata hivyo, Arafati kwenye uchangiaji wake hakusita kusema namna ambavyo hamasa ya Rais Samia Suluhu Hassan ilivyochochea kufanya vizuri kwa timu zetu huku akitoa wito kwa timu nyingine ambazo zitapata nafasi ya namna hiyo kufanya makubwa msimu ujao na isiishie kwa Simba na Yanga

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’