Matumaini ya kumpata Atsu akiwa hai yafifia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Feb 2023
Matumaini ya kumpata Atsu akiwa hai yafifia

Wakala wa Christian Atsu ametangaza taarifa za kuvunja moyo baada ya kupatikana kwa pea mbili za viatu vya Atsu kwenye kifusi nchini Uturuki.

Mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle na Chelsea alionekana mara ya mwisho akiwa nyumbani kwake huko Kahramanmaras ndani ya jengo ambalo liliangushwa na tetemeko la ardhi.

Kupitia mtandao wa Twitter, Wakala Nana Sechere amesema;

"nipo kwenye eneo lilipokuwa jengo alilokuwa akiishi Atsu, nipo na familia yake, tukiendelea kumtafuta, mpaka sasa tumefanikiwa kulipata eneo sahihi kilipokuwa chumba chake na tumepata pea mbili za viatu vyake"

Itakumbukwa kuwa muda mchache baada ya kutokea kwa tetemeko hilo taarifa zinazosadikiwa kutolewa na Makamu wa Rais wa klabu ya Hatayaspor aliyokuwa akiichezea zilisambaa kwa kasi Kimataifa zikieleza kuwa Atsu amepatikana akiwa na majeraha.

Hata hivyo siku moja baadae wakala wake alitoa taarifa kuwa hana mawasiliano yoyote na mchezaji huyo na anaendelea kumtafuta.

Mkanganyiko huu wa taarifa umeleta mgogoro mkubwa kati ya klabu ya Hatayaspor na wakala wa Atsu.

"Uokoaji unakwenda taratibu sana, msaada mkubwa bado unahitajika, pia tunahitaji watafsiri wa lugha, inasikitisha klabu yake hawapo hapa kusaidiana nasi" aliongeza Sechere

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
45m ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
2h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
3h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
9h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
10h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’