Simba kwenda Morogoro leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Apr 2018
Simba kwenda Morogoro leo
Asubuhi ya leo Ijumaa kikosi cha Simba kinaratajiwa kuianza safari ya kutoka Iringa kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumatatu, April 09.

Simba iliweka kambi ya siku mbili mkoani Iringa baada ya mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Njombe Mji.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema waliamua kubaki Iringa ili kutoa nafasi kwa wachezaji kujifua katika mazingira ya baridi ambayo ni bora zaidi ukilinganisha na hali ya hewa ya Dar es Salaam.

Djuma amesema ligi imeingia katika hatua ya lala salama na wanahitaji kuona wachezaji wote wanakuwa tayari kwa mapambano kwa ajili ya kuchukua pointi tatu kila wanaposhuka uwanjani.

"Umefika muda wa hatari, tunahitaji kuonyesha vitendo uwanjani, kule ndio kunaongea zaidi"

Aliitaja Mtibwa Sugar kuwa ni moja ya timu ngumu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara na kwa sababu hiyo wataingia uwanjani kwa tahadhari huku wakiwaheshimu wapinzani wao muda wote wa mchezo.

"Kama tulivyocheza kwa heshima dhidi ya Njombe Mji, tutaendelea kufanya hivyo tutakapocheza na Mtibwa Sugar, tofauti ni majina, lakini wote tunacheza ligi moja na unaposhinda unapata pointi tatu," Djuma aliongeza.

Baada ya mechi hiyo, Simba itarejea jijini Dar es salaam kuwasubiri Mbeya City na Tanzania Prisons, mechi zote zikipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Simba ndio vinara wa ligi kuu ya Vodacom yenye timu 16 wakiwa na pointi 49 ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 46 wakati mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC ambao keshokutwa wataikabili Mbeya City jijini Mbeya wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 40.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’