Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva aliyekuwa anaumwa kwa muda mrefu, leo Alhamisi amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi yake.
Aveva amehudhuria kesi inayomkabili ambapo jana alipaswa kusomewa maelezo ya awali na mwenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Lakini kesi hiyo imeahirishwa na Hakimu Simba hadi Aprili 12, 2018 baada ya Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kubadilisha hati ya mashtaka.
Wakili Swai aliiomba mahakamani hapo kubadilisha hati ya mashtaka kwa kumuongeza mshtakiwa mwingine na kwamba siku hiyo ya Aprili 12,2018 washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Mbali na Aveva mwingine anayekabiliwa na kesi hiyo ni Godfrey Nyange maarufu Kaburu ambaye ni Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.
Washtakiwa hao wapo mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE