Murshid, Nyoni na Kotei kuikosa Mtibwa Sugar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
5 Apr 2018
Murshid, Nyoni na Kotei kuikosa Mtibwa Sugar
Timu ya Simba itawakosa wachezaji watatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya timu hiyo kumaliza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji juzi kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Wachezaji ambao watalazimika kushuhudia mchezo huo wakiwa jukwaani ni Erasto Nyoni, James Kotei na Juuko Murshid ambao wana kadi tatu za njano kila mmoja.

Akizungumza mjini Iringa jana, kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma, alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo, lakini watapambana kupata ushindi.

Nyoni, Kotei na Murshid ni wachezaji wa kikosi cha kwanza na kukosekana kwao ni pigo kwa Simba katika mchezo huo.

Djuma amesema kuwa Simba ina idadi kubwa ya wachezaji, hivyo nafasi zao zitajazwa na wengine aliodai ana uhakika watacheza kwa kiwango bora.

“Kweli inaweza kuwa shida, lakini tutajipanga kuangalia wachezaji gani watacheza katika nafasi zao, kubwa tunataka pointi tatu ni mchezo muhimu kuliko kitu chochote,” alisema Djuma.

Pia Simba inaweza kumkosa beki wa kati Salim Mbonde aliyeumia goti katika mchezo huo wa juzi ambao Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco.

“Itabidi nipate siku mbili za kapumzika nione kama naweza kurudi uwanjani kufanya mazoezi au nipumzike zaidi, lakini kweli nilijitonesha goti, “ alisema Mbonde.

Simba jana ilikwenda kuweka kambi Iringa na Ijumaa inatarajiwa kwenda Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Jamhuri.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →