Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco amesema kwa sasa akili zao zipo kwenye ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakihitaji kushinda kila mechi ili kutimiza malengo yao hayo.
Bocco aliyasema hayo baada ya kuisaidia Simba kushinda 2-0 katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC Jumanne Uwanja wa Saba Saba juzi.
Siku hiyo, mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC alifunga mabao yote, moja kila kipindi Simba SC ikipata ushindi mzuri wa ugenini na kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa.
Mshambuliaji huyo mkongwe amesema licha ya kupata ushindi katika mchezo na Njombe lakini hawatabweteka na kuhakikisha wanapambana kupata pointi tatu muhimu.
“Tunashukuru kupata pointi tatu muhimu katika mchezo na Njombe, tunasahau na kuelekeza akili zetu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar," alisema.
Bocco alisema kikosi chao kipo vizuri kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi na kufikia malengo yao ya kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu.
Simba iliondoka Njombe jana asubuhi kurejea Iringa kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Morogoro kwa mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Jumatatu Uwanja wa Jamhuri.

ADVERTISE HERE