FT : Njombe Mji 0-2 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Apr 2018
FT : Njombe Mji 0-2 Simba
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba wamezidi kutakata kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya leo kuichapa Njombe Mji mabao 2-0 kwenye mchezo wa 'kiporo' uliopigwa kwenye dimba la Sabasaba mkoani Njombe.

Licha ya mazingira mabovu ya uwanja, hayakuizuia Simba kupata ushindi muhimu ambao sasa umewafanya wawe kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 49.

Mabao yote ya Simba yalifungwa na nahodha wa kikosi hicho John Bocco kwenye kila kipindi cha mchezo.



Alianza kuifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya 17 baada ya kushi lake la chinichini alilopiga akiwa nje ya 18 kumshinda mlinda lango wa Njombe David Kissu.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi kwenye kipindi cha kwanza, vijana wa Njombe Mji walikosa mbinu za kuipenya ngome imara ya Simba iliyocheza kwa tahadhari kubwa leo.

Bocco aliiongezea Simba bao la pili kwenye dakika ya 64 baada ya kuunganisha vyema krosi ya Shomari Kapombe kutoka winga ya kulia.

Ushindi huo umeiimarisha malengo ya Simba ya kutwaa ubingwa msimu huu wakati kwa upande wa Njombe Mji hali yao inazidi kuwa tete.

Njombe Mji imesalia nafasi ya 15 ikiwa na alama 18.

Katika mchezo huo kiungo wa Simba Haruna Niyonzima alirejea dimbani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na majeruhi.

Aidha Beki Salim Mbonde naye alirejea dimbani katika kikosi cha Simba baada ya majeruhi ya muda mrefu hata hivyo aliumia tena kwenye mchezo huo.

Mbonde aliingia kuchukua nafasi ya Kotei aliyeumia ;akini naye akashindwa kumaliza mchezo baada ya kuumia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’