Samatta amuongeza makali Kichuya kuelekea mpambano wa watani wa jadi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
1 Apr 2018
Samatta amuongeza makali Kichuya kuelekea mpambano wa watani wa jadi
Siku chache kabla ya mchezo wa watani wa jadi, winga wa Simba, Shiza Kichuya, amepewa darasa la nguvu na Mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta, ambalo linaweza kuleta ‘msiba’ kwa mashabiki wa Yanga wakati timu zao zitakapokutana Aprili 29, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaweza kutoa picha ya ubingwa, kwani timu itakayoshinda itakuwa na nafasi kubwa kutwaa taji hilo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Kichuya, aliyekuwa miongoni mwa wachezaji walioichezea timu ya Taifa, Taifa Stars, mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alisema kuwa, baada ya kipute hicho, alifanya mazungumzo ya nguvu na Samatta, anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Kichuya alisema mbali ya kupongezwa na Samatta kutokana na kiwango alichokionyesha katika mchezo huo, pia alitakiwa na mwenzake huyo kuongeza juhudi na heshima kwa makocha ili atimize malengo aliyojiwekea.

“Alitaka kujua mipango yangu katika soka, nilipomueleza, aliniambia niongeze juhudi uwanjani na heshima katika benchi la ufundi, kwani tayari nimeshaonyesha nina muda mfupi wa kuwapo Tanzania.

“Sitaweza kuweka kila kitu nilichozungumza naye, kwani mengine natakiwa kuyafanyia kazi, nimemuahidi kuyafanyia kazi yote aliyoniambia, yeye ni mkubwa kiumri, amenitangulia kucheza na pia ana mafanikio zaidi yangu, hivyo ushauri wake nitaufanyia kazi,” alisema.

Kutokana na ‘sumu’ aliyopewa na Samatta, Kichuya anaweza kucharuka kwa kufanya mazoezi kwa bidii mno, hali inayoweza kuziponza timu atakazokutana nazo hivi karibuni, ikiwamo Yanga.

Kichuya amekuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba wanaoogopewa na timu pinzani, kutokana na cheche zake awapo uwanjani, zaidi ikiwa ni chenga, umahiri wake wa kupiga pasi na krosi murua za mabao, lakini pia kufunga.

Winga huyo timu yake ya Simba inapokutana na Yanga, amekuwa akiwaliza mara kwa mara watani wao hao wa jadi, tena akifunga mabao ya kiufundi mno.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →