Kiungo Haruna Niyonzima na beki Salim Mbonde wameanza kujifua na kikosi cha Simba baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.
Wachezaji hao wanakaribia kabisa kuanza kuitumikia Simba. Sasa wanafanya mazoezi ya kuirejesha miili yao katika hali ya ushindani.
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amevutiwa zaidi na kiwango cha Haruna Niyonzima baada ya kumuona akilisakata gozi la n'gombe mazoezini kwa mara ya kwanza.
Niyonzima aliumia kabla Lechantre hajakabidhiwa mikopa ya kuinoa Simba.
Lechantre amefurahia kurejea kwa kiungo na kueleza kuwa ataongeza upana wa kikosi chake.
"Nimefurahi kwa kurejea kikosini kwa wachezaji hawa, alisema Lechantre.
"Kwetu ni jambo zuri kwa sababu tunakuwa na upana wa wachezaji na hata katika mechi zetu itakuwa rahisi, bado wanaendelea na mazoezi mepesi nafikiri siku mbili tatu tutakuwa nao".

ADVERTISE HERE