Mkude asema ataivaa Njombe Mji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Mar 2018
Mkude asema ataivaa Njombe Mji
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude, amesema kuwa anaendelea vyema na yuko tayari kuitumikia timu yake katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Njombe Mji FC itakayofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Mapema wiki hii Mkude alipata maumivu katika eneo karibu na enka na kulazimika kutolewa nje ya uwanja, lakini tayari amesharejea kuanza kujifua na wachezaji wenzake.

Akizungumza jana, Mkude, alisema kuwa anaendelea vyema na amewataka mashabiki wa vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokuwa na wasiwasi wowote juu yake.

"Naendelea vizuri, niko vyema na mechi ya Njombe Mji nikipangwa nitacheza," alisema kiungo huyo.

Simba imeondoka jijini Dar es salaam leo. Itaweka kambi ya muda Iringa na baadaye kuanza safari ya kuelekea Njombe Mji kuikabili timu hiyo ambayo iko katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Baada ya mchezo huo, Simba itawafuata Mtibwa Sugar katika mechi nyingine ya ligi itakayofanyika Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’