Uhamiaji bado wanachunguza uraia wa Kidao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Mar 2018
Uhamiaji bado wanachunguza uraia wa Kidao
Uraia wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao bado unachunguzwa na Idara ya uhamiaji imefahamika.

Jana Afisa Habari wa Uhamiaji Ally Mtanda alisema taarifa itatolewa kwa wanamichezo wote baada ya zoezi hilo kukamilika.

"Bado tunaendelea na suala lake la uchunguzi na litakapokuwa tayari tutawaarifu, masuala ya uchunguzi hatuwezi kuyaweka wazi hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha ndipo mambo yote yatakuwa hadharani," alisema afisa huyo.

Kidao amekuwa akituhumiwa kuwa sio raia wa Tanzania na taarifa za uchunguzi wa uraia wake zimekuwa zikizungumzwa mara kwa mara.

Rais wa TFF Wallace Karia naye aliwahi kuingia kwenye mkumbo huo wa kuchunguzwa na Idara ya Uhamiaji kabla ya uchaguzi Mkuu wa TFF uliofanyika August 2017.

Uhamiaji walithibitisha kwamba ni raia wa Tanzania.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’