Timu kadhaa zimeendelea kujitokeza kumuwania winga wa Simba Shiza Kichuya ambaye yuko kwenye kiwango bora wakati huu.
Aidha kiwango alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya DR Congo kimezidi kumtengenezea mazingira mazuri kwani sasa anawaniwa na moja ya timu vigogo wa Afrika, TP Mazembe.
Taarifa za uhakika ni kwamba viongozi wa TP Mazembe ambao walikuwa kwenye msafara wa timu ya Taifa ya Congo, wameanza mchakato wa kumsajili Kichuya.
Viongozi wa Simba pia wako katika mchakato wa kumshawishi kiungo huyo mshambuliaji asaini mkataba mpya kwani mkataba wake umebakisha miezi miwili tu.
Kichuya anaruhusiwa kufanya maongezi na klabu yoyote sasa kwa kuwa mkataba wake uliobaki ni chini ya miezi sita.

ADVERTISE HERE