Manara azungumzia majeruhi kikosi cha Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Oct 2017
Manara azungumzia majeruhi kikosi cha Simba
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amezungumza na waandishi wa habari leo ambapo ameanika hali ya majeruhi katika kikosi cha Simba.

Manara amesema Simba ina majeruhi wanne ambapo watatu hawataweza kucheza mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga Oktoba 28.

Wachezaji hao ni Said Mohammed 'Nduda', Shomari Kapombe na Salim Mbonde.

Nduda amefanyiwa uoasuaji wa goti hivi karibuni nchini India na anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nane, Mbonde aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar na anatarajiwa kuwa nje kwa mwezi mmoja.

Nahodha msaidizi John Bocco yeye alipata maumivu ya kisigino katika mchezo uliopita na atakuwa nje kwa wiki moja.

"Beki wetu Mbonde katika mechi ya Mtibwa alipata maumivu ya goti ambayo yatasababisha kukosa mechi nne ambazo kati yake itakuwa dhidi ya Yanga," amesema Manara.

"Kapombe ni mchezaji tunaamini atatusaidia kwani bila shaka hakuna mpenzi wa Simba asiyefahamu uwezo wa mchezaji huyo ambaye alianza kuonekana akiwa hapa, kwahiyo tunaomba mashabiki wetu, wavumilie juu ya hilo"

"Kipa Nduda atakuwa nje kwa wiki nane ili kupona kabisa na kuanza mazoezi na kuangalia kama anaweza kujiunga na timu au kuendelea na matibabu zaidi ya hapo."

Manara alisema mechi dhidi ya Njombe itakuwa ya kulipiza machungu ya sare waliyoyapata katika mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa sugar.

Katika hatua nyingine viongozi wa Simba wameupongeza uongozi mpya wa bodi ya ligi iliyochaguliwa Jumapili ya wiki iliyopita.

"Tunaimani Bodi hii itakuwa ya huru na haki kwani tunafahamu Mwenyekiti wake aliyechaguliwa Clement Sanga atakuwa anafanya uamuzi ya huru na haki," alisema.

"Tunafahamu kuwa Sanga ni kiongozi wa juu wa Yanga ila kwa uadilifu na ufanisi wake wa kazi tunaimani itakwenda kufanya kazi ya bodi ya ligi bila ya kubezi upande wa Yanga au Simba na kila timu itapata kile ambacho itakuwa inastahili kutoka kwa bodi hiyo," alisema Manara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
7h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
7h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
10h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’