Lechantre ameshawasoma Yanga, wasubiri kipigo tu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
29 Mar 2018
Lechantre ameshawasoma Yanga, wasubiri kipigo tu
Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa, Pierre Lechantre hana presha kabisa na mechi dhidi ya mahasimu wao, Yanga.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wanaendelea kujifua vikali ili kuiangamiza Njombe Mji na kuondoka na pointi tatu kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Imeelezwa kuwa ushindi dhidi ya Njombe Mji Jumanne ijayo utawapa mzuka zaidi wa kupambania ubingwa na kutibua historia ya Yanga.

Mchezo wa mahasimu hao umepangwa kupigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo mshindi atakuwa ametanguliza mguu mmoja katika vita ya kubeba ubingwa msimu huu.

Simba na Yanga kwa sasa zinakabana kileleni kwa pointi 46 huku Wekundu wa Msimbazi wakiongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, pia wana mchezo mmoja mkononi.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba tayari kocha Lechantre akisaidiana na Masoud Djuma wameanza kuifuatilia Yanga kwa karibu ili kuangalia mbinu za kuithibiti.

Katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti, Lechantre kwa mara ya kwanza amekiri kufuatilia staili ya soka la Yanga hasa kwenye eneo la ushambuliaji linaloongozwa na Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu pamoja na lile la ulinzi ambalo linaongozwa na Kelvin Yondani.

“Wana timu nzuri kwa muda niliyoiona, ina wachezaji wengi wazuri tofauti na maeneo ambayo nimeyataja, lakini si muda sahihi kuwazungumzia kwa lolote,” alisema.

“Akili yetu ipo kwa Njombe na nyingine kabla kuikabili Yanga, lakini nitaendelea kuiangalia zaidi katika maeneo hayo mawili ili kuona mambo ambayo yatatupa faida tukikutana.

“Najua mechi ya Yanga ni ngumu na nimeshaambiwa hilo, lakini itakuwa vyema kupata kwanza pointi tatu katika kila mechi ambayo ipo mbele yetu na baada ya hapo tutafanya maandalizi ya kutosha kwa Yanga.

“Kwa sasa natangeneza timu ya kucheza soka la haraka na pasi na sitataka mchezaji kukaa na mpira muda mrefu, hiyo ndio njia nzuri ya kucheza kwa sasa.”

OKWI, BOCCO USIPIME

Kwa upande wake, Djuma alisema malengo yao ni kuchukua ubingwa, lakini watatangeneza mfumo wa kuwatengenezea nafasi nyingi za kufunga kinara wa mabao, Emmanuel Okwi na John Bocco ili mmoja wao aibuke mfungaji bora. Okwi ana mabao 16 mpaka sasa.

“Nadhani itapendeza pale tunapochukua ubingwa na mfungaji bora atoke Simba, hayo ni malengo ambayo tumejiwekea msimu huu, na nina imani tunaweza kuyatimiza,” alisema Mrundi huyo.

“Kama Okwi na Bocco wakiwa wanatamani kufunga katika kila mechi zilizobaki, inaweza kuwa faida kwetu kupata pointi tatu ambazo tunazihitaji.

“Lakini, kufunga ni jambo la nafasi, hata kama Kichuya aliyefunga saba au mchezaji mwingine yeyote klabuni tunampa nafasi, hiyo yote ni katika kuona namna Simba inavyokuwa bingwa msimu huu.”

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →