TFF kumjadili Wambura Jumamosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Mar 2018
TFF kumjadili Wambura Jumamosi
Hatma ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, inatarajiwa kujulikana keshokutwa Jumamosi baada ya kikao cha Kamati ya Rufani ya shirikisho hilo kukutana, imefahamika.

Wambura alikata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa maisha kujishughulisha na soka na Kamati ya Maadili ya TFF baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu yaliyokuwa yanamkabili.

Taarifa kutoka TFF zinaeleza kuwa maandalizi ya kikao hicho yako katika hatua za mwisho na wajumbe wa kamati hiyo tayari wameshapewa taarifa.

"Rufaa itasikilizwa Jumamosi," alisema kwa kifupi kiongozi mmoja wa shirikisho hilo.

Wambura ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF), alihukumiwa adhamu hiyo kwa kuzingatia kifungu cha 73 (1), kifungu cha 73 (7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013 na Ibara ya 50 (1) ya Katiba ya TFF ya mwaka 2015 baada ya kupatikana na hatia na makosa yote yaliyokuwa yakimkabili.

Kosa la kwanza la Wambura lilikuwa ni kupokea fedha za shirikisho hilo ambazo malipo yake hayakuwa halali, kughushi barua na la tatu ni kuishushia hadhi TFF.<

Wakati huo huo, TFF imewasilisha barua kwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ikitaka mwanachama wake, Wakili, Emmanuel Muga, kuacha kumtetea Wambura kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi.

TFF ilisema katika barua yake kuwa, inapinga Muga, kuendelea kumwakilisha Wambura katika mashauri yanayoendelea kwa sababu wakati kiongozi huyo anatenda kosa, wakili huyo alikuwa mwanasheria wa shirikisho hilo chini ya Rais, Jamal Malinzi.

Tayari Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Jumamosi iliyopita, ilimteua, Athumani Nyamlani kuwa Kaimu Rais mpaka pale mkutano mkuu utakapofanyika na kuamua vinginevyo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’