Baada ya kung'ara kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya DR Congo, jana kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya amesema sasa anahamishia makali yake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Njombe Mji unaotarajiwa kupigwa mkoani Njombe, April 03.
Kichuya alifunga moja ya bao katika mchezo dhidi ya Congo ambao Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kichuya pia alitengeneza bao la kwanza lililofungwa na Mbwana Samatta.
Kiwango cha Kichuya kwenye mchezo huo kiliwavutia wengi akiwemo Afisa Habari wa Simba Haji Manara.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Manara alimwagia sifa kedekede Kichuya huku akimfananisha na mshambuliaji hatari wa FC Barcelona Lionel Messi 'La Pulga'.
Tayari wamechazi wa Simba waliokuwa kwenye kikosi cha Stars wamejiunga na wenzao wanaojifua kwenye uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es salaam.
Wachezaji hao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Shiza Kichuya.

ADVERTISE HERE