Kiungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude ambaye juzi aliumia mazoezini na kuibua hofu kwa kikosi cha Simba, anatarajiwa kurejea mazoezini kesho.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema baada ya kufanyiwa vipimo, imebainika kuwa Mkude alipata majeraha ya michubuko ya kawaida.
Amesema hakuna wasiwasi juu ya afya yake na atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachotarajiwa kusafiri kwenda mkoani Njombe kuivaa Njombe Mji April 03.
Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo.
Wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa wanatarajiwa kujiunga na wenzao baada ya kukamilika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Stars dhidi ya DR Congo.
Mchezo huo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa uliishuhudia Stars ikiondoka na ushindi wa mabao 2-0 Shiza Kichuya akin'gara katika mchezo huo kwa kufunga bao moja na kutengeneza jingine

ADVERTISE HERE