Kipa wa pili wa Simba, Said Mohammed 'Nduda' atakuwa nje kwa miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita nchini India.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba Nduda anaendelea vizuri baada ya upasuaji huo na sasa atapumzika kwa wiki nane kabla ya kuanza mazoezi mepesi.
Ikumbukwe Nduda aliyesajiliwa Simba Julai mwaka huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, hajacheza mechi yoyote msimu huu kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata Agosti mazoezini.
Aliumia kambini visiwani Zanzibar wakati Simba inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Mlinda lango huyo tayari amerejea kutoka nchini India alikofanyiwa upasuaji wa goti.

ADVERTISE HERE