Stars yainyoa DRC uwanja wa Taifa, yaichapa 2-0

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Mar 2018
Stars yainyoa DRC uwanja wa Taifa, yaichapa 2-0
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo imewatoa kimasomaso Watanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulio kwenye kalenda ya FIFA uliishuhudia Stars ikicheza kandanda safi ya kujilinda na kushambulia tofauti na mchezo uliopita.

Mabao yote ya Stars yalipatikana katika kipindi cha pili wafungaji wakiwa Mbwana Samatta na Shiza Kichuya.



Samatta alifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 74 akiunganisha vyema krosi ya Shiza Kichuya aliyekuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya DR Congo.

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha DR Congo iliyokuwa imesheheni wachezaji wanaocheza soka Ulaya wakijaribu kusaka bao la kusawazisha.

Hata hivyo walijikuta wakipachikwa bao la pili kwenye dakika ya 86 baada ya Saimon Msuva kuunasa mpira kutoka mguuni mwa kiungo wa DR Congo katikati ya uwanja na kufanya shambulizi la kushitukiza.



Msuva alimpasia mpira nahodha Mbwana Samatta ambaye alimtengenezea Kichuya aliyeujaza mpira wavuni kwa shuti kali la chinichini akiwa nje kidogo ya 18.

Ushindi huo umerejesha ari ya mashabiki wa Stars ambao walianza kukata tamaa na timu yao hasa baada ya kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Algeria.

Mashabiki wengi leo walijitokeza kwenye uwanja wa Taifa kuipa sapoti Stars. Uhamasishaji pamoja na viingilio 'rafiki' vimechangia wananchi wengi kwenda uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo huo.

Kiingilio kwa upande wa VIP ilikuwa Tsh 5,000/- wakati mzunguuko ikiwa ni Tsh 1000/- tu.

Matokeo hayo yataisaidia Stars kupanda katika viwango vya FIFA mwezi ujao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’