Njombe Mji yaomba mchezo dhidi ya Simba usogezwe mbele

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Mar 2018
Njombe Mji yaomba mchezo dhidi ya Simba usogezwe mbele
Uongozi wa Njombe Mji umesema kuwa umepeleka mapendekezo kwa shirikisho la soka nchini TFF kuomba mchezo wake dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika April 03 upangiwe tarehe nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msemaji wa klabu hiyo, Hassan Macho imesema klabu ya Njombe Mji inatakiwa kuwa mkoani Shinyanga March 30 kucheza Stand United mchezo wa robo fainali kombe la FA.

Licha ya safari ya kwenda Shinyanga kupangwa leo, timu hiyo bado haijaondoka ikisubiri muafaka juu ya maombi yake.

Hii hapa taarifa ya Njombe Mji

Timu ya Njombe Mji FC inapenda kuujulisha umma wa Wananjombe na wapenda soka nchi nzima kuwa, tumepeleka mapendekezo yetu TFF na bodi ya ligi kuhusu taarifa ya ratiba tuliyoipokea jana saa 10 jioni ikionyesha mchezo kati yetu na simba utachezwa tarehe 3 Aprili 2018.

Katika mapendekezo yetu tumeishauri yafuatayo kwa TFF na TPBLB:-

1. Baada ya michezo iliyokuwa kwenye ratiba inatoa nafasi katika kipindi cha siku 12 baada ya mchezo na Azam tarehe 15 Aprili, ingependeza mchezo ungechezwa hapo, badala ya kiporo cha Simba na Kagera Sugar kingefaa kuchezwa tarehe 3 mwezi wa 4 kwa timu zote hizo hazishiriki FA Cup.

2. Kama ni lazima Simba icheze kiporo hiki basi mchezo huo tumependekeza ufanyike tarehe 30 au 31 mwezi wa tatu na mchezo wetu wa FA uliotakiwa kuchezwa tarehe 30 uchezwe tarehe 4.

Kwa kuwa barua yetu imefikishwa TFF na bodi ya ligi tunasubiri maamuzi ya busara kutoka TFF.

Ikumbukwe timu ilitakiwa kusafiri tarehe 27.3.2018 tukaamua kusitisha safari ili kwanza tupate muafaka.

Majibu yote yatapatikana baada ya barua kupata majibu.

Tuwaombe Wananjombe kuwa watulivu kipindi hiki ambacho tunashughulikia hali hii.

Imetolewa na
Hassan Macho
Msemaji wa Njombe Mji FC
27.3.2018
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’