Okwi hauzwi - Uongozi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
26 Mar 2018
Okwi hauzwi - Uongozi Simba
Uongozi wa Simba, umedai kuwa hauwezi kumuuza mchezaji wao Mganda, Emmanuel Okwi kwa timu ya Al Masry na umesisitiza kuwa sasa wa­nawaza kuhusu ubingwa na siyo kuuza wachezaji.

Okwi ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea timu ya Sports Club Villa ya kwao Uganda kwa ada ya shilingi milioni 115, ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa nayo 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa mwenye 12.

Katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry, ilielezwa kuwa Waarabu walivutiwa na ‘udambwi­udambwi’ wa Mganda huyo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Said Tully, alisema kuwa kwa sasa wanachoweza kuwaza ni kuhusu mechi zao kumi zilizobakia kwenye ligi kuu, masuala ya kuuza wachezaji bado muda wake, ila kuhusu taarifa za kutakiwa na Al Masry hawajaweza kuzungumza nao suala hilo.

“Tumebakiwa na me­chi kumi hivyo mipango yetu na mikakati yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote na kuweza kuchukua ubingwa lakini pamoja na ushindani wa kwenye ligi tunajua kuwa kuna makosa nyuma timu imefanya na kuweza kushindwa kupata pointi lakini sisi kama uongozi tumeji­panga kuhakikisha kuwa makosa hayo hayajirudii na hakuna njia ny­ingine zaidi ya kufanya maandalizi ya kutosha na kuweza kushinda mechi zote.

“Hakuna maongezi yoyote tuliyofanya na Al Masry kuhusu kumuuza Okwi na huu siyo muda wa kuuza wachezaji na agenda yetu namba moja sasa hivi ni kush­inda ligi na kuchukua ubingwa na hatuwezi kuzungumza masuala yoyote, hivyo tutazung­umza hilo msimu ukiwa ushamalizika, sasa hivi agenda yetu ni kupam­bana kama tukiweza kuchukua ubingwa au tukishindwa ndiyo tut­ajua nani tumuuze nani tubaki naye,” alisema.

Championi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →