Baada ya kuzidhibiti Simba na Yanga, Katwila atamba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
17 Oct 2017
Baada ya kuzidhibiti Simba na Yanga, Katwila atamba
Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kwamba hawajazibana Yanga na Simba Dar es Salaam kwa kubahatisha, bali ni sehemu ya mkakati wao wa kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.

Mtibwa Sugat ilitoa sare ya 1-1 na Simba SC jana wiki mbili tu baada ya kutoa sare ya 0-0 na Yanga, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa jana, Mtibwa walitangulia kwa kwa bao la Stahmili Mbonde dakika ya 35 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopagwa na beki wa zamani wa Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, kabla ya wenyeji kusawazisha kwa bao la mpira wa adhabu la Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 90 na ushei.

Akizungumza jana baada ya mchezo, Katwila alisema kwamba mchezo dhidi ya Simba ulikuwa mgumu, lakini waliingia na mkakati wa kupata bao la mapema ili kuwanyong’onyesha wapinzani wao.

“Katika mchezo huu tulikuja na lengo la kupata bao la mapema kutokana na kuwatambua wapinzani wetu na tunashukuru tulifanikiwa katika hilo, bahati mbaya wakati tunaamini tunashinda, wenzetu wakapata bao la kusawazisha, ila tunashukuru kupata pointi moja ugenini si jambo ndogo,” alisema.

Katwila alisema anatambua timu kubwa za Simba na Yanga ukiingia kucheza nazo lazima uanze kwa tahadhari ya hali ya juu, ili kuepuka kuwapa nafasi ya kuanza kukufunga.

Lakini Katwila pia akasema bao la kusawazisha la wapinzani wake, lilitaka kuwavuruga vijana wake kwa sababu lilikuja wakiwa wanaamini wamekwishashinda mechi.

“Goli la Simba la kusawazisha lilifungwa katika wakati mbaya, wachezaji wangu walijua wamekwishashinda, kwani muda ulikwishaenda sana, hvyo imewaumiza sana na kusababisha wazozane wao kwa wao kutokana na kuonekama kama kuna mmoja alifanya makosa,” alisema.

Katwila alisema kama kocha aliwatuliza vijana wake na kuwaambia mambo kama hayo hutokea katika michezo, hivyo wasahau yaliyopita na kuelekeza nguvu zao katika mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →