Kulingana na gazeti la Burudani na Michezo la Championi, Mzabuni wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ubÂingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifanikiÂsha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara ameliambia gazeti hilo kuwa huo ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji kuipambania timu yao kutwaa ubÂingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma.
“Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo.
“Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuongeÂza hamasa kwa wacheÂzaji,†alisema Manara.
Naye kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefungukia juu ya michezo yao hiyo 10 iliyobakia amÂbapo alisema:
“Mechi hizi 10 zilizobakia siyo nyingi sana, kikubwa ambacho tunatakiÂwa kukifanya ni kuendeÂlea kupigana tupate pointi kwa kila mechi.â€

ADVERTISE HERE