Huu hapa mpango mkakati wa ubingwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
23 Mar 2018
Huu hapa mpango mkakati wa ubingwa Simba
Kulingana na gazeti la Burudani na Michezo la Championi, Mzabuni wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ub­ingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifaniki­sha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara ameliambia gazeti hilo kuwa huo ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji kuipambania timu yao kutwaa ub­ingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma.

“Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo.

“Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuonge­za hamasa kwa wache­zaji,” alisema Manara.

Naye kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefungukia juu ya michezo yao hiyo 10 iliyobakia am­bapo alisema:

“Mechi hizi 10 zilizobakia siyo nyingi sana, kikubwa ambacho tunataki­wa kukifanya ni kuende­lea kupigana tupate pointi kwa kila mechi.”
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →