Simba kurejea mazoezini kesho, akili yote kwenye ubingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Mar 2018
Simba kurejea mazoezini kesho, akili yote kwenye ubingwa
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema watautumia vyema muda ambao timu hiyo haina mechi za kimataifa na Kombe la FA kurekebisha makosa ya kiufundi waliyoyabaini ili warejee kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na kasi.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi kesho Jumamosi kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Saba Saba mkoani Njombe.

Djuma, amesema wanataka kuona hawapotezi pointi katika mechi zao tisa zilizobakia na hatimaye wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Djuma amesema wana lengo la kukiimarisha zaidi kikosi chao kwa sababu hatua iliyobaki ni ngumu zaidi kutokana na vita ya kuwania ubingwa na ile ya kushuka daraja kufanana.

"Tunaelekea mwisho wa ligi, huku ni kugumu zaidi na ndio tunahitaji kushinda, ukipoteza pointi, basi umempa nafasi mpinzani wako, hatutaki kuona tunapoteza hii nafasi iliyobaki ya kushinda taji msimu huu," alisema kocha huyo raia wa Burundi.

Aliongeza kuwa mechi zote zilizobaki kwenye ligi ni ngumu na wanawakumbusha wachezaji wao kutobweteka au kuingia uwanjani na matokeo ya mzunguko wa kwanza.

Kikosi hicho kinachoongozwa na Mfaransa, Pierre Lenchatre, kimerejea kwenye Ligi Kuu kamili baada ya kuondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Al Masry ya Misri ambayo ililazimisha sare ya mabao 2-2 walipokutana Machi 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kutoka suluhu ugenini.

Simba ndio inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16 ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana pointi 46, lakini wakizidiwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku Azam FC wenye pointi 40 wakiwa katika nafasi ya tatu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’