FT : Algeria 4-1 Tanzania

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Mar 2018
FT : Algeria 4-1 Tanzania
Algeria imeendeleza ubabe kwa Tanzania baada ya leo kushinda mabao 4-1 kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa nchini humo.

Mchezo huo uliokuwa kwenye kalenda ya FIFA uliishuhudia Algeria ikitawala kwa muda mwingi na iliandika bao la kuongoza mapema kwenye dakika ya 13 mfungaji akiwa Baghdad aliyepokea pasi mpenyezo kutoka kwa Riyad Mahrez.

Stars iliyocheza kwa kujihami zaidi na kushambulia kwa kushitukiza ilisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 20 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya kutua kichwani kwa Saimon Msuva na kuujaza wavuni kwa urahisi.

Mashambulizi mfululizo ya ALgeria kwenye lango la Stars yalipelekea walinzi wa Stars kufanya makosa ya mara kwa mara ambapo kwenye dakika ya 43, beki Shomari Kapombe alijikuta akiutumbukiza kimiani mpira wa krosi katika jitihada za kuokoa.

Kipindi cha pili ALgeria iliendelea kutawala na kujipatia mabao mengine mawili kupitia kwa Baghdad na Medjan.

Matokeo hayo yanaifanya Algeria iendeleze ubabe dhidi ya Tanzania kwani huo ni ushindi wa pili mfululizo baada ya mchezo uliopita kushinda kwa mabao 7-0 kwenye dimba hilo hilo.

Stars inarejea nchini kujiandaa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya DR Congo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa, March 27 2018
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’