Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho, Simba inalazimika kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu ili ipate nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
Simba tayari ilishaondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC) ambalo ilitwaa msimu uliopita na kupata tiketi ya kushiriki kombe la Shirikisho msimu huu.
Akizungumza juzi kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Simba John Bocco amesema nguvu zao zote wanazihamishia katika ligi na watahakikisha wanatwaa ubingwa.
"Tutahakikisha nguvu hii tuliyokuwa nayo kwenye michuano ya kombe la Shirikisho tunaihamishia kwenye ligi," alisema Bocco.
"Tunatambua ukubwa wa Simba na tutahakikisha tunatwaa ubingwa wa VPL msimu huu. Tunafahamu bila ya kutwaa ubingwa hatutakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao."
"Tunarejea nyumbani tukiwa imara kutimiza azma ya kutwaa ubingwa tulioukosa kwa misimu kadhaa."
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi Jumamosi ijayo. Wachezaji walipewa mapumziko ya wiki nzima baada ya mchezo dhidi ya Al Masry.

ADVERTISE HERE