Benchi la Ufundi linavyomsaidia Mavugo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Mar 2018
Benchi la Ufundi linavyomsaidia Mavugo
Mshambuliaji Laudirt Mavugo raia wa Burundi alikuwa mchezaji wa kutumainiwa kwenye kikosi cha Simba katika msimu wake wa kwanza.

Simba ilifanya kazi ya ziada kunasa sahihi yake wakati huo akiwa mchezaji hatari kwenye ligi ya kwao huko Burundi.

Katika msimu wake wa kwanza, Mavugo aliifungia Simba mabao nane kwenye ligi kuu ya Vodacom.

Hata hivyo Mavugo amekuwa akipungua makali siku hadi siku hadi kupelekea mashabiki wa Simba kukosa imani nae wengine wakipendekeza aachwe.

Mavugo nusura aachwe kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Novemba mwaka jana, usajili wake wa mkopo kwenda Gor Mahia ya Kenya ulikwama kwenye dakika za mwisho.

Lakini tangu kuwasili kwa kocha Pierre Lechantre, Mavugo amekuwa akipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba mara nyingi akitokea benchi.

Tangu siku zake za mwanzo Lechantre alionekana kuvutiwa na mshambuliaji huyo kutokana na kipaji alichonacho lakini pia alibaini mapungufu yake.

Moja ya mahojiano yake na waandishi wa Habari, Lechantre alisema Mavugo ni mchezaji hatari lakini tatizo lake kubwa amepoteza kujiamini.

Hivyo kwa kushirikiana na benchi lake la Ufundi, Lechantre alisema wanajaribu kumsaidia kuondoa tatizo hilo ili awe mchezaji wa kutegemewa.

Bila shaka kazi ya benchi la ufundi imeanza kuzaa matunda. Mavugo amekuwa akibadilika taratibu, ameanza kuonyesha makali yake.

Licha ya kukosa nafasi ya wazi kwenye mchezo dhidi ya Al Masry nchini Misri Jumamosi iliyopita, Mavugo ndiye aliyeongeza kasi ya mashambulizi ya Simba na kuwapa wakati mgumu Al Masry waliolazimika kutumia mbinu ya kujiangusha mara kwa mara.

Bila shaka naye amebaini kilichokuwa kinamkwamisha na sasa huenda huu ukawa mwanzo mpya kwa mchezaji huyo ambaye alisajiliwa kwa 'mbwembwe' mwaka juzi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’