Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi Jumamosi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Njombe Mji.
Simba inayoongoza ligi kwa tofauti ya mabao dhidi ya mahasimu wao Yanga, itasafiri mkoani Njombe kuikabili Njombe Mji kwenye mchezo huo wa kiporo ambao uliahirishwa ili kuipa nafasi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika baada ya kumalizika kwa mapumziko ya Michuano ya Kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA.
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre alisafiri kwenda Ufaransa baada ya mchezo dhidi ya Al Masry na anatarajiwa kuwasili mapema kabla ya kuanza kwa mazoezi siku ya Jumamosi.

ADVERTISE HERE