Lechantre kuisuka upya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
20 Mar 2018
Lechantre kuisuka upya Simba
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amedokeza kuwa mwishoni mwa msimu anakusudia kukisuka upya kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

Lechantre amesema msimu huu ukimalizika atakifumua kikosi na kuvuta nyota wapya sita ili kukifanya kitikise michuano ya kimataifa.

Lechantre amesisitiza Simba inahitaji mabadiliko zaidi.

Amesema anaona wachezaji kama John Bocco na Emmanuel Okwi, lakini tatizo ni kwamba kuna wengine ni kama mizigo kwa kushindwa kuisaidia timu hiyo.

Mfaransa huyo aliyewahi kuzinoa kwa mafanikio timu za taifa za Cameroon na DR Congo alisema kwa hali ilivyo anahitaji nyota wapya sita watakaoweza kuibadilisha timu na kuifanya iwe na makali ndani na nje ya nchi na si kuangalia Ligi Kuu pekee.

Alisema pamoja na maeneo mengine, watalazimika kuboresha safu yao ya kiungo pamoja na washambuliaji.

“Kwa ujumla tunahitaji wachezaji wenye uwezo wa kucheza mechi za ndani na hizi za kimataifa. Tukikosa kwenye Ligi ya ndani tutalazimika kutafuta wa kutoka nje,” alisisitiza.

Alisema Bocco na Okwi ambao wamefunga mabao 34 kwenye mashindano yote msimu huu, wanaitendea haki nafasi hiyo lakini tatizo ni kwamba hawana mbadala, endapo wawili hao wakikosekana kwa pamoja.

“Ukiwakosa Bocco na Okwi unachanganyikiwa, ukitazama kwenye timu hakuna mchezaji mwingine wa kukubeba. Hawa ni wachezaji hatari si tu hapa Tanzania, bali Afrika.

“Tunahitaji kuwa na wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa kama wao au zaidi. Mavugo (Laudit) ni mzuri lakini tulipofika hapa hakuwa fiti hata kidogo, walau sasa tunamsaidia,” alisema Lechantre.

Kwa upande wa kiungo alisema waliopo sasa wengi sasa ni washambuliaji hivyo wanahitaji kupata viungo wengine wa kusaidia kukaba.

“Tunahitaji pia wachezaji wa kukaba zaidi. Tuna viungo wengi wazuri lakini kwenye kushambulia. Wengi wakipoteza mpira hawasaidii sana kwenye kukaba, hiyo ndiyo sababu wakati mwingine tunalazimika kumtoa James Kotei kwenye beki na kumpanga kiungo,” alisema Lechantre.

Katika upande mwingine, Lechantre alisema kuna baadhi ya wachezaji ambao timu hiyo italazimika kuachana nao mwishoni mwa msimu kwa kuwa hawana uwezo wa kuitumikia timu hiyo.

“Kuna wachezaji hapa wana uwezo wa kawaida, unashangaa imekuwaje wako Simba. Si kwamba hawajitumi, hapana, ila sio wa daraja la Simba, Simba ni timu kubwa,” alisema.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →