Karia akerwa na 'upigaji' TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
20 Mar 2018
Karia akerwa na 'upigaji' TFF
Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa atafanya kazi bila woga kwa sababu anataka kumaliza ubabaishaji katika shirikisho hilo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Karia, alisema kuwa anaamini kwa kufanya hivyo atarejesha heshima ya TFF na hatakuwa tayari kuona mtu yoyote anachezea fedha za shirikisho hilo hata kama atakuwa ni rafiki yake.

Karia aliongeza kuwa hatorudi nyuma katika mapambano hayo na yuko tayari hata kutolewa kafara lakini atapambana bila woga kuondoa ubabaishaji na udhalimu TFF.

“Nimeombwa sana mambo yanayofanyika kwenye Shirikisho nisiyapeleke kwenye kamati husika tukae mezani tuyazungumze sitakaa meza moja na mdhalimu mimi,” alisema.

Alisema kamati zilizoundwa ni huru na hivyo hata kama ni yeye amefanya mambo kinyume na maadili apelekwe.

“Hata kama ni mimi nimefanya udhalimu nipelekwe kama Blatter, nimesimamia halmashauri mimi, miaka yote sijafanya mambo ya udhalimu ingawa mimi pia ni binadamu na nina mapungufu yangu lakini sio kwenye masuala ya fedha,” alisema.

“Nawaambia kabisa watu mimi ni Magufuli (John- Rais wa Tanzania) pale waulize watumishi wangu Mvomero pale, Magufuli alipoingia madarakani walikuwa wanamwita Karia, sasa jiulize kwa nini walimwita hivyo, sina masikhara kwenye fedha za taasisi,” alisema.

Karia alikwenda mbali zaidi kuhusu kamati za TFF na kusema: “Ukikuta mtu amehukumiwa na kamati hizi hakubali basi ujue kuna walakini… tusome katiba zetu mimi nilivumilia miaka minne ya Malinzi (Jamal- Rais wa zamani wa TFF) sikumlaumu alivyokuwa akifanya kwa sababu ni suala la kikatiba nilimlaumu kuninyima nafasi yangu tu kama mwenyekiti wa kamati ya fedha maana hatukuwa tukikaa vikao,” alisema.

“Na lazima mjue yote haya nayafanya kwa maelezo ya Fifa, Fifa ilizuia fedha za maendeleo tangu mwaka 2015, 16 na 17 baada ya kutokea yale yaliyokea nyote mnayajua (Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa kufikishwa mahakamani).

Alisema baada ya tukio hilo, Fifa walisitisha fedha zote na kutoa masharti kama TFF inazihitaji waondoe makandokando ikiwa ni pamoja na kuruhusu ukaguzi ufanyike.

“Baada ya sintofahamu ya wenzetu, Fifa walikuja kufanya ukaguzi kuanzia mwaka 2013 na wakagundua mambo mengi hivyo lazima mjue mambo yote yanafanyika kwa maagizo yao,” alisema.

Alisema kama wakitekeleza matakwa ya Fifa na kuondoa makandokando wanatarajia kupata dola za Marekani milioni tatu.

“Na kuna dola nyingine laki moja na sabini kwa ajili ya kugharamia tiketi kwa timu za taifa pia kuna dola laki 4 kwa vifaa, tangu nipo TFF sikuwahi kuzisikia hizo fedha kumbe zipo… nataka mambo yote yaendeshwe kwa uwazi,” alisema.

Mbali na hayo, Karia alisema katika kipindi chake cha miezi saba amefanikiwa kuendesha mashindano mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.

Alimaliza kuwa TFF imeendesha mashindano ya Kombe la Azam, Ligi Ndogo, Nane Bora ya Wanawake, Soka la Ufukweni na kuahidi kurekebisha pale kwenye mapungufu.

Kauli ya Karia, imekuja siku chache tu baada ya kamati ya maadili kumfungia kutojihusisha na soka maisha, Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura, kwa tuhuma za kufoji malipo pamoja na kulitia aibu shirikisho hilo

IPP Media
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →