Mandawa aongezwa kikosi cha Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Mar 2018
Mandawa aongezwa kikosi cha Stars
Mshambuliaji Mtanzania, Rashid Mandawa anayeichezea klabu ya BDF XI ya Botswana, Rashidi Mandawa ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Stars inajiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taifa Stars itaanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria Machi 22 2018, kabla ya kuikaribisha nyumbani timu ya taifa ya Kongo, Machi 27 2018.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, awali aliita kikosi chenye jumla ya wachezaji 23 lakini baadhi wamepunguzwa kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.

Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na Shaban Idd.

Kikosi hicho kinaelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kirafiki utakaopigwa Mach 22 2018.

KIKOSI KAMILI
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’