Simba ikiendeleza 'kasi ya Kimataifa' ubingwa mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Mar 2018
Simba ikiendeleza 'kasi ya Kimataifa' ubingwa mapema
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirkisho barani Afrika, kikosi cha Simba kinarejea jijini Dar es salaam leo.

Simba imeondoshwa kwenye michuano hiyo kwa faida ya mabao ya ugenini iliyopata Al Masry katika mkchezo uliopigwa kweye uwanja wa Taifa, March 07.

Kilichowafurahisha wengi ni kiwango cha hali ya juu kilichoonyeshwa na Simba kwenye michezo yote miwili dhidi ya Al Masry.

Ni vigumu kuamini Simba imeyaaga mashindano hayo kwani haikupoteza mchezo wowote lakini ni sheria za michuano hiyo zilizofanya iondoshwe kwenye raundi ya kwanza.

Sasa inarejea Tanzania kuendeleza ubabe katika ligi kuu ya Vodacom ikiwa bado inaongoza kwa tofauti ya mabao huku pia ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Jana Afisa Habari wa Simba ambaye ni shabiki namba moja wa wekundu wa Msimbazi, Haji Manara alitamka bayana kuwa kwa Simba aliyoiona ikipambana Misri, haoni timu ya kuizuia isitwae ubingwa msimu huu.

Manara alikwenda mbali zaidi kwa kuahidi kwamba kama Simba haitatwaa ubingwa msimu huu basi atapumzika kwa muda kufuatilia masuala ya soka.

Hakika, Simba ile iliyoizuia Al Masry kwenye dimba lao haipaswi kukosa ubingwa wa VPL.

Kukosa ubingwa utakuwa ni uzembe!

Kwanza Simba itakuwa na mashindano ya ligi pekee huku wapinzani wake wakikabiliwa na mashindao zaidi ya moja.

Azam FC inashiriki kombe la FA pia wakati Yanga itabanwa na ratiba ya kombe la FA pamoja na kombe la Shirikisho barani Afrika.

Hivyo Simba itakuwa na muda zaidi wa kujiandaa na michezo ya ligi kuliko wapinzani wake.

Pili Simba ndio timu bora. Naamini matokeo ya hivi karibuni katika ligi yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji kuweka nguvu zaidi kwenye michuano ya Kimataifa.

Simba haijafungwa msimu huu, imebaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi.

Inahitaji kuendeleza mwenendo huo kwa kushinda michezo yake yote iliyobaki ili kuwapa furaha mashabiki wake ambao wamekuwa nayo bega kwa bega katika hali zote.

Ubingwa wa VPL utaiwezesha Simba kushiriki michuano ya klabu bingwa Barani Afrika mwakani lakini kama haitatwaa ubingwa mwakani haitashiriki michuano yoyote ya Kimataifa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’