Tulikosa bahati Misri - Djuma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Mar 2018
Tulikosa bahati Misri - Djuma
Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema hawakuwa na bahati ya kusonga mbele katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika waliyokuwa wakishiriki.

Simba imetolewa na Al Masry kwa faida ya mabao ya ugenini waliyopata katika sare ya magoli 2-2 huku mechi ya marudiano iliyofanyika juzi mjini Port Said timu hizo zikitoka suluhu.

Djuma amesema wachezaji walicheza katika kiwango cha juu sambamba na wapinzani wao lakini hakuna upande uliofanikiwa kupata bao katika mchezo huo.

Djuma amesema juzi aliona wachezaji wa Simba wakicheza soka la nidhamu na umakini tofauti na wanavyocheza katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo wao ni vinara.

"Kiukweli imetuuma sana kutoka katika mashindano ya CAF (Shirikisho la Soka Afrika), wachezaji walipambana kadri ya uwezo wao ili kutafuta bao, juhudi zao zilikuwa za kiwango cha juu, ila mwisho wa siku katika mpambano ni lazima mmoja awe mshindi, lakini katika mechi hii wenzetu walikuwa na bahati," alisema Djuma.

Kocha huyo raia wa Burundi aliongeza kuwa watakaa na wachezaji na kuwaambia wasahau michuano hiyo na sasa nguvu walizoonyesha kwenye mashindano hayo ya kimataifa wahamishie kwenye Ligi Kuu ili watimize ndoto zao za kutwaa ubingwa msimu huu.

"Tumebakia na ligi ya nyumbani peke yake, akili na nguvu zote ni kuchukua ubingwa, ule wakati tuliwaza mashindano matatu, hatutaki kuona tunapoteza ubingwa, tunajua mechi zilizobaki za kuamua ubingwa," aliongeza Djuma.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’