Wakongwe Simba, Yanga wapongeza sapoti ya mashabiki Misri na Botswana

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Mar 2018
Wakongwe Simba, Yanga wapongeza sapoti ya mashabiki Misri na Botswana
Nyota wa zamani wa Simba na Yanga wameonyesha kufurahishwa na mashabiki wa Tanzania waishio ughaibuni wanavyozisapoti timu zao nje ya nchi bila kujali Usimba na Uyanga unaoziangusha timu hizo zikicheza nyumbani.

Frank Kassanga 'Bwalya' na Sylvanus Ibrahim 'Polisi' waliwapongea Watanzania waishio Botswana na Misri walivyoziunga mkono timu za Tanzania katika mechi zao za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho bila ubaguzi kama unaofanywa nchini.

"Waliopo Botswana bila kujali Usumba na Uyanga waliishangilia Yanga na kutoka suluhu ni kama waliopo Misri, bila kujali ni mashabiki wa Yanga, waliunga mkono Simba kwa kujua wanaiwakilisha Tanzania, kama mashabiki wa jijini Dar wangebadilika ingezisaidia timu zetu kwa mechi za nyumbani." alisema Kassanga.

Naye Polisi alisema;

"Wanaoishi Misri na Botswana, wametufumbua macho, kama kweli tumeamua timu zetu zinaposhiriki michuano ya kimataifa, tusiwape nafasi wageni kupata ujasiri kama vile wanacheza nyumbani kwao, tubadilike kwani zinatuangusha."

Hata hivyo, Boniface Pawasa nyota wa zamani wa Simba, alisema kinachowafanya Watanzania wanaoishi nje wawe wazalendo kwa Simba na Yanga, zilipocheza ugenini ni kwa kutoziona siku nyingi, hivyo kuziunga mkono tofauti na waliopo Dar.

"Ila uzalendo wao, unawatia moyo wachezaji kujiona sio wapweke, hii iwe funzo kwa mashabiki waishio Tanzania, kuacha kujipendekeza kwa wageni," alisema Pawasa

"Nyie Wanahabari mna nguvu ya kutoa elimu kwa mashabiki, kujua utaifa ni nini na kujua athari za kuwaunga mkono wageni, kunashusha hadhi ya soka la Tanzania".

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’