Wekundu wa Msimbazi, Simba wameyaaga mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kutoa suluhu ya 0-0 dhidi ya Al Masry katika mchezo wa marudiano baina ya timu hizo uliopigwa Port Said nchini Misri.
Al Masry imesonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya kuilazimisha Simba sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Taifa March 07.
Kocha Pierre Lechantre alibadili mfumo wa kikosi chake leo ambapo aliweka viungo wengi waliosaidia katika ulinzi huku wakitumia mashambulizi ya kushitukiza.
Baada ya kujilinda kwa muda mrefu Simba ilicharuka katika dakika 15 za mwisho kwa kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Al Masry.
Hata hivyo bahati haikuwa upande wa Simba na mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya 0-0.
Baada ya kutolewa katika michuano hii, sasa Simba ina kazi moja tu ya kuhakikisha inatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ili ipate nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
Simba itakuwa na muda wa kutosha kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu kwani ndio mashindao pekee itakayokuwa inashiriki wakati wapinzani wake katika mbio za ubingwa, Yanga na Azam FC zote zina mashindano ya kombe la FA huku Yanga ikikabiliwa na mashindano matatu.

ADVERTISE HERE